
Shirikisho la soka Tanzania limeliandikia barua shirikisho la soka Africa kuomba mchezo wa Biashara United dhidi ya Al Ahli Tripoli usongezwe mbele hadi Jumanne ijayo badala ya kesho jumamosi.
Shirikisho limeeleza kuwa,limepolea maelekezo ya waziri mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa yaliyowataka wahakikishe Biashara United inaenda Libya kecheza mchezo wa marudiano wa kombe la Shirikisho (CAF) dhidi ya Al Ahli Tripoli.
Shirikisho limeweka wazi kuwa tayari Serikali imetoa ndege ya kuwasafirisha Biashara United lakini tatizo liliopo mpama sasa ni kupatikana kwa vibali vya kuruhusu ndege hiyo kutua Sudan ikiwa inaelekea Libya.
