
Kocha mkuu wa klabu ya Simba Sc kwenye michwano ya (CAF) Hitimana Thierry amesema, kesho watajitahidi kucheza kwa kuwafurahisha mashabiki huku wakiwa makini kulinda ushindi.
Hitimana amekiri kuwa klabu ya Simba hivi karibuni haichezi mpira wa kuvutia lakini kikubwa ni kupata ushindi.
Aidha,,kocha wa klabu ya Jwaneng Galaxy Morena Ramoreboli ameonesha kukata tamaa kwa kusema,hawataupa kipaumbale sana mchezo wa kesho dhidi ya Simba Sc.
Amesema mchezo huo dhidi ya Simba Sc atakutumia Kama pre-season kuelekea michezo yao ya ligi.
Amesema,focus yao kubwa itakuwa kwenye mchezo wa ufunguzi wa ligi kuu ya Botswana ambayo ilisimama kwa karibu mwaka mmoja sasa..
