Klabu ya Simba imeonesha kukubali kuwa msimu huu ni ngumu kutetea taji la ligi kuu ya NBC baada ya watani wao wa jadi kuwa kileleni kwa tofauti ya alama 13 mpaka sasa.
Mtendaji mkuu wa Klabu hiyo Barbara Gonzalez amekiri kuwa Simba kwasasa wamehamishia nguvu zao kwenye Kombe la Shirikisho ambapo wanategemea kucheza mchezo wa nusu fainali jumamosi hii dhidi ya Yanga.
“Kwenye ligi tunacheza kukamilisha ratiba,Lakini nafasi ya Ubingwa kwa upande wetu Sasa iko kwenye FA” Alisema Barbara Gonzalez.
