
Tamko la klabu ya Young Africans SC kuhusu adhabu waliyopewa na (CAF)
Klabu ya Yanga SC kupitia kwa msemaji wao Haji Manara umesema kuwa wao hawatapingana na Shirikisho la soka (CAF) ikiwa adhabu itaelezea na kufafanua kuhusu adhabu husika
Klabu ya Yanga SC imesema itaandika barua CAF kuomba ufafanuzi kwa sababu wao hawaoni sehemu waliyokiuka taratibu.
Amesema,kuhusu tukio la kucheleshwa kutolewa kwa vyeti vya COVID-19 vya Wachezaji wa River’s United,wao hawahusiki kwa sababu Yanga SC haimpimi COVID-19 hilo sio jukumu lao ni jukumu la serikali.
“Hi sheria ya wapi hiii!! Yanga SC sisi ndo tunapima COVID-19?! Tutaandika barua CAF.” ~Haji Manara
Kuhusu virugu alizofanyiwa afisa habari wa River’s United klabu ya Yanga SC imesema wao hawahusiki wanashangaa,kwa sababu waliohusika kumzuia ni walinzi wa uwanja wabTaifa ambao ni waajiriwa wa Serikali,wao Kama Yanga Hilo suala haliwahusu.
Kuhusu kuingiza mashabiki uwanjani,,,klabu ya Yanga SC imesema wao waliotoa taarifa siku moja kabla ya mchezo kuwa mashabiki hawaruhusiwi kuingia uwanjani.
Na siku mchezo hakuna mashabiki wa Yanga SC waliooingia uwanjani, waliooingia ni maafisa wa klabu hiyo ambao wanaruhisiwa kuingia.
Amesema wenye jukumu la kuzuia mashabiki ni (TFF) na sio Yanga kwa sababu uwanja wa taifa sio wa Yanga SC, Yanga jukumu lao ni kutoa taarifa na walifanya hivyo kabla
Amesema wataandika barua kupitia (TFF) wakiridhishwa na majibu watalipa faini,wao hawakatai kulipa faini ila wanataka walipe faini halali isiyo na uonevu ndani yake
