Nyota wa Klabu ya Us Gendarmerie ya nchini Niger, Victorien Adebayor ameweka wazi hatma yake kuelekea msimu ujao
Nyota huyo amekuwa akiwindwa na vilabu kadhaa barani Afrika huku hivi karibuni taarifa zimekuwa zikimhusisha kufikia makubalino na Mabingwa wapya wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika Klabu ya RS Berkane ya nchini Morocco.
Hata hivyo nyota huyo ameweka wazi kuwa anataka kucheza Simba Sc ya nchini Tanzania msimu ujao.
“Nataka kucheza Simba msimu ujao, nataka kujiunga na timu ambayo kweli itahitaji mchango wangu na kuthamini kipaji changu, kuhusu Berkane sio wao tu, timu nyingi zinanihitaji lakini lazima niwe makini sana..” Amesema Adebayor.
Simba inamhitaji Adebayor kwa udi na uvumba hasa baada ya nyota wake Bernard Morisson kuhusishwa kusaini kwa mahasimu wao Yanga.
