Michuano ya mataifa ya Afrika inayoendelea nchini Cameroon imefikia ngazi ya kumi na sita Bora(mtoano).
Baada ya wiki mbili ya mechi za makundi hatimae timu 16 zimefanikiwa kutinga hatua hii. Katika hali isiyotarajiwa na wengi mabingwa watetezi Algeria imetupwa nje katika hatua ya makundi baada ya kupata point moja katika kundi lake. Timu nyingine iliyoshangaza Ni Ghana waliotolewa katika kundi lao.

Katika hatua hii ya mtoano wenyeji Cameroon watamenyana na Comoros, huku Burkinafaso wakicheza dhidi ya Gabon, Malawi watamenyana na Morocco.
Nigeria ndo timu pekee iliyoshinda michezo yake yote mitatu ya makundi. Je watafanikiwa kushinda michezo yote Hadi kubeba kombe ? Michezo ya hatua ya mtoano itaanza kuchezwa siku ya jumapili.
