
Wikiendi hii katika Ligi kuu nchini Uingereza imeshuhudiwa mitanange ya kukata na shoka .
Tukianza na mechi za jumamosi. Arsenal imeendelea kuimarika baada ya kuifunga Leicester city mabao 2-0 bila na kuipandisha the Gunners hadi nafasi ya sita katika .
Katika mechi nyingne Manchester city inayoongozwa Pep Guardiola ikapokea kichapo cha mabao 2-0 dhidi ya Crystal Palace na kuwaweka vijana wa Guardiola pointi tano nyuma ya vinara Chelsea.
Nao Chelsea wameendelea kujikita kileleni baada ya kuishindilia magoli 3-0 dhidi ya Newcastle matajiri wapya wa Ligi kuu ya Uingereza.
Majogoo wa jiji Liverpool nao wakatoa sare ya mabao Mawili (2-2) dhidi ya Klabu ya Brighton. Na katika mechi kubwa ya wikiendi Klabu ya Manchester United imeweza kuifunga Klabu ya Tottenham mabao matatu kwa bila na kufanikiwa kuinusuru kibarua cha kocha wao Ole Gunnar.
Kwa Jana jumapil tumeshuhudia Klabu za Norwich na Astonvilla zikiendelea kutepeta baada ya kufungea hapo Jana. Norwich walifungwa mabao Mawili kwa moja dhidi ya Leeds United huku Astonvilla akifungwa mabao 4-1 dhidi ya Westham.
