
Tetesi za Usajili na uhamisho Barani Ulaya
Moja kwa moja tuanzie London Uingereza,klabu ya Manchester United imeungana na vilabu vingine,vikiwemo Arsenal, Tottenham Hotspur na Newcastle United kutaka saini ya Mshambuliaji Mserbia Susan Vlahovic,21 kutoka Fiorentina.
Paris St-Germain imefanya mazungumzo na kocha was zamani wa Real Madrid,Zinedine Zidane wakijiweka sawa na uwezekano was kocha wao Mauricio Pochettino kuondoka na kujiunga na Manchester United.
Kiungo was Lazio Sergio Milinkovic- Savic, 26, anawaniwa na Manchester United Kama mbadala was Paul Pogba, amabaye mkataba wake na klabu hiyo Old Trafford unakwenda kumalizika mwishoni mwa msimu.
Tuhitimishe taarifa zetu nchini Italia katika klabu ya Intermilan Mkataba was Wings was Croatia Ivan Persic pale Inter Milan unakwisha June 2022 na nyota huyo mwenye umri wa miaka 32 anasema
“chochote kinawezakana,ngoja tuone wiki Chache zijazo” alipoulizwa kuhusu mustakabali wake.
Pia klabu hiyo inamatumaini kwamba kiungobwake Mcroatia Marcelo Brozovic,29 atasaini mkataba mpya, kwani mkataba wake wa sasa unamalizika mwishoni mwa msimu huu.
