
Baada ya wadau,wepenzi na mashabiki wa soka Nchini Nigeria kulalamika kutokana na kukosekana kwa jina la Ademola Lookman 24 anayepiga katika klabu ya Leicester City ya nchini Uingereza.
Kwenye kikosi Cha mwisho chenye jumla ya majina ya wachezaji 28 wa timu ya Taifa hilo kitakachoshiriki mashindano ya AFCON yanayotarajiwa kufanyika mwakani mwezi January mpaka February.
Shirikisho la soka nchini humo limesema kuwa nyota huyo Bado hajaidhinishwa na shirikisho la soka duniani,FIFA kuiwakilisha Nigeria katika ngazi ya kimataifa lakini bado mchakato mzima was kubadili uraiawake unaendelea.
“Jina lake llijumuishwa kwenye orodha ya awali ya muda ya wachezaji 40 kwa Imani kwamba mchakato ungekuwa umekamilika.”
Ukumbukwe Lookman tayari amezitumikia timu za vijana za England ambavyo ni chini ya umri was miaka 29,20 na 21. Lakini kwa Sasa ameamua kuitumikia timu ya Taifa ya Nigeria ambako ndipo wazazi wake walipozaliwa na kabla hawajaenda kusaka maisha nchini Uingereza.
