Leo jumanne na kesho jumatano michuano ya Klabu bingwa barani ulaya itaendelea. Michezo hii Ni ya mwisho katika hatua ya makundi huku baadhi ya timu bado hazijui hatma zao katika michuano hio.
Leo itachezwa michezo ya kundi A hadi kundi D.
Katika kundi A Klabu ya Manchester city itawakaribisha Leipzig katika mchezo wa kumaliza ratiba. Manchester city washafuzu hatua ya mtoano na ndio vinara wa kundi A. Mchezo Mwingine wa kundi A utawakutanisha matajiri wa Paris Klabu ya PSG watakaomenyana na Club Brugge. PSG wapo kwenye shinikizo kutokana na matokeo mabovu waliopata hivi karibuni katika michezo ya Klabu bingwa na pia michezo ya Ligi kuu nchini ufaransa.
Katika kundi B kutakua na michezo ya kukata na shoka. Liverpool ndo kinara wa kundi na ameshajihakikishia nafasi katika hatua ya mtoano huku vilabu vingine katika kundi hili wakiwa na nafasi ya kufuzu hivyo michezo ya leo ndo itakayoamua. Ac Milan wapo San Siro watawakaribisha Liverpool huku FC Porto wakicheza dhidi ya Atletico Madrid.
Katika kundi C Ajax na Sporting Lisbon wameshafuzu hatua ya mtoano hivyo mechi za Leo Ni ya kukamilisha ratiba tu.
Na mechi ya mwisho kwa leo itakua kutoka kwa kundi D. Real Madrid na Inter Milan wameshafuzu. Klabu ya Sheriff nayo imefanikiwa kwenda kwenye michuano ya Europa.
