Baada ya taarifa kutoka kamati ya uendeshaji na usimamizi wa ligi ya Bodi ya ligi kuu ya Tanzania kuitaka mamlaka ya uteuzi wa Mjumbe Jemedari Said Kazumari kutengua uteuzi wake kisha kupeleka shauri lake kwenye kamati ya maadili kutokana na kuchapisha video na picha kisha kuweka maelezo yanayoishusha hadhi ligi kuu kwa kuiita dhaifu
Jemedari Said ameandika kwenye ukurasa wake wa Instagram
“Kuna jamaayangu anaitwa @dizomoko (Mdidi the Writer) aliwahi kuniambia. “…. we Mzee hizo akili zako tunza utatumia mahali pengine….”
NB: Ni Hatari sana kuwa na Akili katikati ya Kundi la wajinga.
BIN KAZUMARI.”
Tanzania kumekuwa na mjadala mkali kuhusu ubora wa ligi yao huku wengine wakisema ligi ni dhaifu, wengine wakisema ni bora huku wengine wakisema sio dhaifu wala sio bora ispokuwa imepiga hatua
