Kuelekea mchezo wa kesho wa ligi kuu ya NBC Kati ya Azam Fc dhidi ya Simba, Msemaji wa Azam Zakaria Thabit (Zaka Zakazi) amewaonya Simba kutofanya waliyoyafanya Afrika Kusini.
Zaka amewaambia Simba wasiwashe Moto kwenye uwanja wa Chamazi kwakuwa kuna gari linatumia mafuta ya ndege.
“Tunawaomba Simba wasiwashe moto pale Kwetu kuna gari letu,Gari ambayo inatumia mafuta ya ndege ambayo yanadaka kwa haraka sana moto hivyo tunawaomba sana Simba wakija wasije kuwasha moto wataleta madhara makubwa sana” Alisema Zaka Zakazi
