Klabu ya Simba imewawaondosha katika benchi la la ufundi, kocha mkuu, kocha wa makipa na kocha wa viungo. Siku mbili baada ya Klabu ya Simba kuondolewa katika michuano ya Klabu bingwa Afrika na timu ya Jwaneng Galaxy ya Botswana kwa kufungwa magoli 3-1 katika uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es salaam. Kocha Didier Gomes amehudumu Simba kwa miezi minane tu na kufanikiwa kufika hatua ya robo fainali ya Klabu bingwa Afrika pamoja na kutetea taji la Ligi kuu na kombe la shirikisho la Azam. Na kocha Gomes ameshinda tuzo ya kocha bora wa msimu wa 2020-2021.
Kwa sasa Klabu ya Simba ipo chini ya kocha Thiery Hitimana kama kocha mkuu, Seleman Matola kama kocha msaidizi hadi pale kocha mkuu mwingne atakapotangazwa. Kesho jumatano Simba itacheza mchezo wa ligi kuu dhidi ya polisi Tanzania.