

Weekend hii ilikua ya kibabe sana katika soka. Tumeshuhudia matokeo ya kikatili na ya kuburudisha kwa wapenda soka kote duniani
Tukianza na Ligi pendwa dunia ni , Ligi kuu nchini Uingereza: Chelsea wameendeleza ubabe wao kwa kuwafunga vijana wa Norwich city kwa mabao 7-0 na kuendelea kujikita kileleni mwa msimamo, Washika mitutu wa London Arsenal nao wameendelea kujitutumia baada ya kupata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Astonvilla siku ya ijumaaa. Nao mabingwa watetezi Manchester city wametoa kichapo cha mabao 4-1 kwa timu ya Brighton and Hove. Siku ya jumapili ndipo ngoma ilipochezwa haswaa. Brentford na Tottenham walifungwa dhidi ya Leicester na Westham. Na jioni ya jumapili ndipo tuliposhuhudia mashetani wekundu wakipewa dhahama ya mabao ndani ya ngome kongwe. Liverpool iliichakaza United kwa mabao 5-0 na kuendelea kuwapa United na kocha wao Ole Gunna wakati mgumu.
Katika Ligi zingine barani ulaya tumeshuhudia Real Madrid wakipata ushindi katika El classico baada ya kuifunga Barcelona mabao 2-1. Ac Milan wakipata ushindi wa mabao 4-2. PSG ikalazimishwa sare pacha na Marseille.