
Klabu ya Manchester United umefanya mazungumzo na kocha Antonio Conte kuhusu Kimrithi mikoba ya Ole Gunnar Solskjaer hii ni kulingana na Sky Sports ya Italia.
Mpaka sasa suala la Ole limewagawa wajumbe wa bodi ya Manchester United baadhi wakitaka aendelee kubaki wengine wakitaka aondoke klabuni.
Mgogoro na mgawanyiko umeingia mpaka kwa Wachezaji wenyewe wa klabu ya Manchester United.
Jana Wachezaji wa timu ya Manchester United hawakufanya mazoezi ya kurejesha mwili katika hali ya kawaida Kama ilivyo ada..baadala yake wamepewa mapumziko wakati bodi ikishughulikua suala la Ole.
