
Kuelekea mchezo dhidi ya crystal palace kocha amezungumzia mambo yafuatayo
Kuhusu majeruhi..
Wachezaji karibia wote ni wazima ukimtoa xhaka ambaye kila mmoja anajua kuwa atakuwa nje kwa miezi mitatu
©anaendelea vyema na matibabu na ninaamini atakuwa fit ndani ya miezi miwili na inaweza isifike mitatu kama inavyotazamiwa
®kuhusu mchezo dhidi ya crystal palace chini ya Patrick Viera
Kila mmoja anajua namna ambaye Patrick alivyokuwa mchezaji muhimu na alikuwa nahodha wa arsenal nategemea atapata mapokezi mazuri
©kuhusu Partey kama atakuwepo kwenye mchezo wa jumatatu
Tutaangalia kama atakuwa hana uchovu atakuwemo kwenyw kikosi bado hatujaamua
©kuhusu kuchaguliwa kuwa kocha bora wa mwezi
Si jambo la MTU mmoja Mimi kushinda tuzo hii ni kazi ya timu nzima imefanyika ndo maana nimekuwa bora
Kuhusu Smith Rowe
Ni mchezaji mzuri ambaye kila siku anaonesha kitu tofauti kwenye kila mchezo
*kuhusu Martneli kwenda kwa mkopo
Hapana Gab bado Nina mipango naye sana atazidi kuwa kwenye kikosi na hatutamtoa kwa mkopo kwenda popote
©Kuhusu Lacazette kuondoka January
Bado ni mchezaji tunayemhitaji na yuko kwenye mipango yetu na tutafanya kila kitu kubaki naye
Kuhusu Wilshire
Tunazidi kufanya naye mazoezi wakati mwingine anafanya na vijana wadogo na hii ni katika kumweka sawa kimazoezi na kiuchezaji
©kuhusu invisible
Ni kikosi kilichofanya makubwa sana kipindi hicho
Kuhusu kauli ya thiery henry kuwa bado hajavutiwa na namna klabu inavyocheza
Arteta amejibu kauli hii kinamna ya pekee
Anasema yeye ndo anaisikia kutoka kwa aliyeuliza swali (mwandishi)na amesema kuwa ni maoni kama yalivyo maoni mengine
