Mfanyabiashara na Muwekezaji wa Simba SC No Dewji ambaye anamiliki 49% ya hisa za Simba SC kwa Thamani ya Tsh Bilioni 20 Jana katangaza rasmi kujiuzulu nafasi yake Uenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ndani ya Simba SC na nafasi yake itachukuliwa na aliyekuwa Makamu wake Salim Abdallah almarufu Try Again, No Dewji amefikia uamuzi huo kutokana na Mara nyingi kutokuwa nchini.
“Mmetuunga mkono kwa miaka minne ya Uongozi wangu Kama Mwenyekiti wa Bodi,kwenye miaka minne tumepata mafanikio makubwa tumeshinda Ligi mara 4 na kufanya vizuri kwenye Champions League muda umefike kama Mohammed na tumekubaliana Mimi nitajiuzulu kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Simba SC naomba sana msifikie kuwa Mimi nimeondoka Simba Sc bali bado ni Muwekezaji”

