Klabu ya Arsenal imeifunga Astonvilla kwa mabao 3-1 katika mchezo wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza. Ushindi huo unawafanya Arsenal kufikisha idadi ya pointi 14 na kuwa nafasu ya 9 kwenye msimamo. Arsenal walianza mchezo kwa kasi na kujipatia mabao Mawili katika kipindi cha Kwanza kupitua kwa Thomas Partey na kapteni Aubameyang. Kipindi cha pili Arsenal waliendea walipoishia na kufanikiwa kupata goli la tatu kupitia kwa kijana wao Emile Smith Rowe. Katika dakika za lala salama Astonvilla walipata bao la kufutia machozi. Goli lilifungwa na kiungo wao mshambuliaji J Ramsey aliyeingia kipindi cha pili.Mechi inayofuata kwa Arsenal ni siku ya jumanne dhidi ya Leeds United katika kombe la Carabao kabla ya wikiendi inayokuja kukutana na Leicester city katika mechi ya Ligi kuu