
Shirikisho la soka nchini Tanzania (TFF) imeiandikia barua shirikisho la soka Afrika(CAF), kuiomba kuisogeza mbele mechi ya kombe la shirikisho barani Afrika kati ya Al ahly Tripoli ya Libya dhidi ya Biashara United hadi jumanne . Hii ni kutokana na changamoto ya usafiri iliyowakabili Biashara United na kushindwa kwenda nchini Libya. Mechi ya awali iliyopigwa Tanzania , Biashara United walishinda kwa mabao Mawili kwa bila(2-0).