
Mzozo mkali umeshuhudiwa baina ya Kenya na Somalia Kuhusu pembetatu ya Kilomita za mraba 38,000 Katika Bahari ya Hindi ambayo inadhaniwa kuwa na utajiri wa mafuta na gesi.Mzozo huo wa kesi mpakani inasemekana kuwa ndio umechangia mzozo wa kidiplomasia Kati ya nchi hizo Majirani.
Kwa muda wa Miongo minne iliyopita,nchi ya Kenya imedai kuwa mstari unaoelekea mashariki mwa mahali ambapo nchi hizo mbili zinakutana pwani zinawakilisha mpaka wa baharini huku Somalia nao wakipinga usemi huo kwamba mpaka wa baharini unapaswa kufuata mwelekeo sawa na mpaka wa ardhi.
Baada ya Jopo la Majaji wanne waliokaa Hague kufuatilia kesi hiyo,ilisemekana kwamba Kenya haijathibitisha kuwa Somalia hapo awali ilikubaliana na mpaka wake uliodaiwa, badala yake walichora laini mpya inayogawanya eneo la mgogoro Mara mbili.
Mwaka wa 2009 nchi hizo mbili za Afrika Mashariki zilikubaliana Katika hati ya makubaliano,ikiungwa mkono na UN,kumaliza mzozo wa mipaka kupitia mazungumzo.Lakini baada ya miaka mitano baadaye Somalia ilidai kuwa mazungumzo yalishindwa na badala yake ikaenda ICJ.Inasemekana kwamba Somalia ilikasirishwa na Kenya kuuza leseni za uchunguzi wa rasilimali za mafuta na gesi Katika eneo lenye mzozo kwa mataifa mawili mnamo 2012.
