
Photo courtesy/Fox
JEURI YA GARETH BALE MAAMUZI MAGUMU YA MESUT, AKUMBUKWE SIMONE! 🏟
_
Mwanafalsafa wa ufaransa, Simone Adolphine Weil aliwahi kusema
“Ikiwa unataka kujua Mwanaume ni Mtu gani. Muangalie jinsi atakavyo react pale anapoona atapoteza Pesa”
Kesho October 13, anafikisha miaka 77 Mrembo huyu tangu atutoke. Nafsi yake izidi kupumzika kwa Amani. Amen 🙏
_
Ni kweli ili kujua mwanaume ni mtu wa aina gani. Muangalie jinsi atakavyofanya mbele ya kupoteza pesa. Always huchukua maamuzi magumu. Maamuzi ambayo kwa sisi wanaume huita ‘Maamuzi ya Kiume’. Ilimradi Pesa zisipotee
.
Muda mchache uliopita nilikuwa na pitia taarifa @goal. Mara nikamuona Mesut Özil. Ndio Mesut Özil. Anaitwa Mesut Mustapha Özil. Raia mmoja hivi wa Ujerumani mwenye asili ya Uturuki
_
Si unakumbuka ule mkataba wa Wajerumani uliosainiwa miaka ya 1960’s. Ukiwaomba Waturuki wakaongeze nguvukazi Ujerumani. Ili kujenga Ujerumani mpya baada ya nchi hiyo kuathiriwa vibaya na Vita ya Pili ya Dunia (WW2)
_
Basi makundi mengi ya raia wa uturuki walikimbilia Ujerumani. Miongoni mwao alikuwepo Babu na Baba yake Mesut Özil. Na hiyo ndio asili ya Mesut Özil kwenda kuzaliwa Ujerumani. Tuachane na hayo.
_
Basi nikasoma majibu ya Mesut Ozil. Akikataa kuondoka Arsenal na kuahidi atabaki Arsenal mpaka mkataba wake utakapoisha June 30, 2021. Nikacheka kidogo 😊
_
Ujue kuna vitu viwili tu vinavyomfanya aendelee kutaka kubaki Arsenal. Kitu cha Pili ni Mashabiki. Alafu na kuna hichi cha Kwanza. Kitu ambacho hata Simone alituambia ukitaka kumjua mwanaume ni mtu gani. Mcheki atakavyo react kwenye kwenye hicho
_
Sio kwamba Mesut Özil hataki kuondoka ukadhani anaipenda sana Arsenal kuliko Jack Wilshere au Vava Voom TH.14. Hapana. Na bado hamfikii Aaron Ramsey, Uncle Thom wala Non-Fly Dutchman. Kwa kuipenda The Gunners.
_
Simaanishi kuwa anakchukia Arsenal. Hapana. Bali hata kama anaipenda lakini hawezi kufikia upendo wa hao niliokutajia. Labda anaipenda Arsenal kuliko Alexis na Frimpong.
_
Amekuwa na nyakati ngumu kikosini lakini kaamua kubaki. Sio kisa anaipenda sana Arsenal. Wala kwa vile anapendwa sana mashabiki wa Arsenal.
_
Mesut amechagua kuendelea kubaki arsenal. Kaona kheri akae nje msimu mzima lakini abakie. Kwa mujibu wa kitambulisho chake cha uraia kinaonesha ndio kwanza ana miaka 31. Na hajali kuhusu kupangwa wala kutokupangwa kwenye kikosi. Unafikiri jeuri yote hii kaitolea wapi? 🙇
_
Mesut jeuri kaitolea hapa. Kwenye haya maisha kwa daraja lake Mesut Özil hana anachodaiwa na Mpira. Labda yeye ndio audai mpira. Kama ni #uefa hata @ronaldo hakuwahi kutwaa na heshima yake milele imebaki palepale. Kama ni Ballon D’or hata Vava Voom hana na heshima yake imebaki palepale
_
Nilikutajia kitu cha pili. Kikabaki kitu cha kwanza kinachomfanya ang’ang’anie kubakii. Pesa. Pesa ndio kitu pekee kinachomfanya Mesut aendelee kubakia @arsenal
.
Kwa daraja lake Mesut ameshashinda kila kitu, tena akiwa kama mtu mwenye mchango mkubwa kwenye mafanikio ya Kitimu kwa kila walichotwaa. Mungu ampe nini tena zaidi?
_
Nafasi ya maneno ni chache, kama tutaanza kuorodhesha mafanikiobya Mesut kuanzia ndani mpaka nje ya 🏟
_
Ila kaa ukijua. Mesut kila mwisho wa wiki anaingiza mshara wa £350,000, takribani Bilioni 1.07 kutoka kwa mwajiri wake. Haijalishi acheze au asicheze. Hata kama wewe ndio Özil. Mungu akupe nini zaidi? Uondoke uende wapi tena?
_
Sio kwamba hakuna timu kubwa zinazomtaka Mesut Özil. Timu zipo. Ila hakuna timu kubwa yeyote ile ambayo ipo tayari kumlipa kiasi hichi cha mshahara kama anacholipwa Arsenal. Ndio maana Mabosi wanamfanyia visa ili aondoke. Waweze kusave kiwango hichi cha mshahara
_
Istoshe, hichi anachokifanya Mesut ndio kile kile kinachoendelea pale Jijini Madrid. Gareth Bale nae akiwa na miaka yake 31 kagoma kuondoka Santiago Bernabeu hadi tamati ya mkataba wake June 30, 2022
_
Yote haya ni sababu Pesa. Bale kwa wiki anapokea mshara wa £600,000. Ni takribani Bilioni 1 na Million 820 za Kitanzania za Kitanzania. Unataka Mungu akupe nini tena?
_
Sishangai. Hichi wanachokifanya Mesut & Bale aliwahi kukifanya Rafiki yangu Malouda 😊. Haya ndo maamuzi magumu. Mtaani tunaita ‘Maamuzi ya Kiume’. Maamuzi ambayo Mwanaume anayafanya ili kuzuia pesa zake zisipotee
