
PICHA/HISANI
Kocha wa Timu ya Taifa Engin Firat ambaye aliteuliwa juzi Kama kocha wa Harambee Stars aanza Safari yake na Vijana hao vibaya Sana hii Ni baada ya kulazwa Mabao Tano kwa nunge na Vijana wa Timu ya Taifa ya Mali.
Harambee Stars ilikuwa na matumaini kabambe ya kuonyesha mchezo mzuri Katika mechi hiyo iliyochezwa usiku wa Alhamisi Tarehe Saba Oktoba 2021.Mechi hiyo ya hatua ya Muondoano wa kusaka tiketi ya kushiriki Katika Kombe la Dunia Mwaka 2022 iliishia kwa Mabao Tano kwa Bila kwa faida ya Vijana wa Timu ya Taifa ya Mali.
Adama Traore aliiweka Timu ya Taifa ya Mali kidedea kwa kufunga bao la kwanza Katika dakika ya Saba muda mfupi tu kabla ya Ibrahima Kone kuipatia Mali bao la Pili dakika ya ishirini na mbili,bao la tatu dakika ya Thelathini na Sita na Kisha la Nne kupiti mkwaju wa Penalti dakika ya 45.Bao la Tano ambalo lilikuwa bao la kumaliza mchezo lilifungwa na Moussa Doumbia dakika ya 85.
Kwenye kipindi Cha Pili Cha mchezo ilimbidi Engin Firat Kufanya badiliko la Mlinda lango ambapo Ian Otieno aliondolewa na Kisha Farouk Shikhalo akaingizwa Mchezoni.
Kwa Sasa Kwenye kundi E Kenya Ni wa Tatu na alama mbili pekee huku Majirani Uganda wakipanda Hadi nafasi ya Pili na alama tano,Mali nao wakiongoza kundi na alama Saba.
Kenya Tena itakabana Koo na Mali Tarehe kumi Oktoba Katika hatua ya Pili ya Muondoano huo wa kufuzu Kombe la Dunia.
