Tottenham Hotspurs imefanikiwa kumsajili nyota wa Brazil Richarlison kwa kiasi cha ada ya pauni milioni 60 kutoka Everton

Nyota huyo wa zamani wa Watford mwenye umri wa miaka 25 akihusika katika mabao 15 kwenye michezo 30 akiwa na Everton msimu uliyopita amesaini mkataba wa miaka mitano kuwatumikia wakali hao wa jiji la London
Richarlison anaungana na Fraser Foster,Ivan Perisic pamoja na kiungo wa Brighton Yves Bissouma kuwa miongoni mwa nyota wapya waliosajiliwa na kocha wa timu hiyo Antonio Conte mpaka sasa.
