Mkurugenzi wa uwekezaji wa Kampuni ya GSM na Mjumbe wa kamati ya usajili wa Klabu ya Yanga Eng.Hersi Said ameweka wazi kile kinachoendelea kati yake na kiungo mtukutu wa Klabu ya Simba Bernard Morisson
Eng.Hersi amesema Yanga ina mpango wa kumsajili nyota huyo raia wa Ghana mwishoni mwa msimu huu pale atakapomaliza mkataba wake na Simba na amekiri tayari wako kwenye mazungumzo na mchezaji huyo.
“… Morrison ni mchezaji mzuri,tunaangalia uwezekano wa kumsajili mwisho wa msimu atakapomaliza mkataba wake na Klabu yake na tayari tumeshaanza mazungumzo naye na ameonesha nia ya kuendelea kubaki Tanzania” Alisema Eng.Hersi
