Nyota watatu wa Klabu ya Al Ahly ya nchini Misri Ali Maaloul,Aliou Dieng na Luis Miquissone wameleta taharuki miongoni mwa mashabiki wa Klabu hiyo baada ya taarifa kutoka kuwa wameitwa na timu zao za Taifa.
Kiungo Aliou Dieng ameitwa kwenye Kikosi cha timu ya Taifa ya Mali kwajili ya kujiandaa na mchezo dhidi ya Dr Congo unaotarajiwa kuchewa June 06 mwaka huu wakati beki wa pembeni wa Al Ahly na timu ya Taifa ya Tunisia Ali Maaloul ameitwa kujiandaa na mchezo dhidi ya Equatorial Guinea utakaopigwa June 02 mwaka huu
Luis Miquissone yeye ameitwa na timu ya Taifa ya Msumbiji kwajili ya kujiandaa na mchezo dhidi ya Rwanda utakaopigwa June 02 mwaka huu pia.
Taarifa hiyo imepokelewa tofauti na mashabiki wa Klabu ya Al Ahly na wameutaka uongozi kukataa kuwaruhusu nyota hao kuondoka klabuni hapo wakati huu.
Al Ahly wanajiandaa na mchezo wa fainali ya Klabu Bingwa Afrika dhidi ya Wydad Athletic Club utakaopigwa May 30 huku hapa katikati ndani ya mwezi huu wakiwa na mechi tatu za ligi kuu ya Misri.
