Ureno yatia mguu mmoja ndani ya kombe la dunia mwezi wa November nchini Qatar baada ya kuwanyuka na kuwatinga nje Uturuki Kwa mabao 3-1. Otavio alifungua karamu ya mabao ya Ureno katika dakika ya kumi na Tano baada ya kupokea pasi kutoka Kwa mchezaji wa Manchester City Bernardo Silva.

Otavio alirudisha mkono Kwa kumtingia pasi ya bao mchezaji wa Liverpool Diogo Jota ambaye hakusita na kutinga bao la pili dakika tatu kabla wakati wa mapumziko. Kipindi Cha pili Uturuki ilijizatiti na kuregesha bao Moja katika dakika ya sitini na Tano kupitia Kwa mchezaji wa Lille ya Ufaransa Burak Yilmaz. Mchezaji wa akiba Nunes Matheus alitinga bao la tatu na la ushindi dakika za mazidadi. Ushindi huo uliiweka Ureno katika nafasi nzuri kufuzu kombe la dunia watakapo shiriki fainali ya kuwania kufuzu.
Katika mchezo mingine North Macedonia iliwashangaza wengi baada ya kuwatinga nje Italia ikiwa nyumbani kwao Kwa kuwashinda Kwa bao Moja Kwa bila. Bao lakeTrajkovski katika dakika ya pili ya mazidadi kipindi Cha pili liliwahakikishia Macedonia nafasi ya kufuzu kombe la dunia Kwa mara ya kwanza. Kipigo Cha Italia kiliwaweka nje ya kombe la dunia Kwa mara ya pili Kwa mfululizo baada ya kukosa kufuzu kombe la dunia mwaka wa 2018.
Mabao mawili ya Gareth Bale yaliihakikishia Wales nafasi ya mchujo kwenye fainali baada ya kuwashinda Austria Kwa mabao mawili Kwa moja. Bao la Quaison R. katika muda ya ziada liliiweka Uswidi kwenye fainali ya mchujo Kwa kuwatinga nje Czech republic. Poland walipata nafasi ya Moja Kwa moja kwenye fainali baada ya wapinzani wao Urusi kupigwa kalamu kutoshiriki kombe la dunia na uongozi wa mpira duniani FIFA.
Kwenye mechi za mchujo fainali Ureno itakutana na N. Macedonia nayo Uswidi itakutana na Poland.