Ligi kuu ya soka nchini Uingereza imefikia nusu ya michezo ya msimu huu. Hadi kufikia Sasa vijana wa Pep Guardiola wanaongoza Ligi hiyo kwa pointi 50 wakifuatiwa na Chelsea wenye alama 42.
Kwa mara nyingi timu inayoongoza Ligi Hadi kipindi cha Christmas na mwaka mpya huibuka kuwa bingwa wa Ligi ifikapo mwezi Mei.
Huku vilabu vikiandamwa na majeruhi pamoja na janga la uviko 19 ikiendelea kusababisha baadhi ya michezo kuahirishwa Klabu ya Manchester city inaendelea kushinda na kuongeza uwiano dhidi ya wapinzani wake.

Kwa top 6 ni Manchester city pekee wana muendelezo mzuri wa matokeo wakishinda michezo yao kumi iliyopita.
Wikiendi hii watakuwa wageni wa Washika mtutu wa London Arsenal. Arsenal na wao wapo kwenye kiwango Bora kabisa na Sasa wanashikilia nafasi ya Nne na wakipata matokeo dhidi ya Manchester city wanaweza isogolea nafasi ya tatu na ya pili.
Mchezo mwingne ni siku ya jumapili Chelsea dhidi ya Liverpool. Mchezo huu unaweza kutoa taswira juu ya kinyanganyiro cha bingwa wa Ligi kuu. Droo itakua na ahueni kwa Manchester city.
Huku Arsenal wakiwa wa Moto, Conte na Spurs yake, United wakijitafuta, Nani kuingia Nne Bora? Na je Liverpool na Chelsea wataweza kumfunga paka kengele?
