Timu ya soka ya Tanzania leo itashuka dimbani kucheza na ni timu ya Congo DRC katika michezo ya kufuzu kombe la dunia nchini Qatar mwakani.
Tanzania wanaongoza kundi lao wakiwa na point 7 na wanahitaji ushindi katika michezo miwili iliyosalia ili waweze kufuzu katika hatua ya mwisho ya kuelekea kombe la dunia mwakani. Watakaoongoza katika makundi ndio wataingia katika kumi bora na kufanya mchujo wa kupata timu tano zitakazowakilisha bara la Afrika katika michuano hiyo mikubwa duniani.
Tanzania wapo kundi moja na timu ya Congo DRC, Benin na Madagascar