Kiungo mshambuliaji wa Klabu ya Arsenal Emile Smith Rowe ameitwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Uingereza kwa ajili ya michezo miwili ya kufuzu kombe la dunia 2022 nchini Qatar.
Bwana mdogo Emile amekua na kiwango kikubwa msimu huu na kuweza kuwasaidia Arsenal kupata point 20 na kuwa nafasi ya tano kwenye msimamo pointi sita nyuma ya vinara Chelsea.
Smith Rowe maarufu kama Croydon KDB ameitwa kuchukua nafasi ya Rashford na James Ward prowse waliojitoa timu ya Taifa kwa sababu mbalimbali.