Klabu ya Simba imemtangaza Pablo Franco kuwa kocha mkuu wa kikosi hicho.
Pablo anachukua nafasi ya Didier Gomes Da Rosa aliyesitishiwa mkataba wake baada ya Simba kutolewa katika michuano ya Klabu bingwa Afrika.
Franco ameshawahi kuwa kocha msaidizi katika Klabu ya Real Madrid chini ya kocha mkuu Carlo Anceloti. Pia ameshakuwa kocha mkuu wa Getafe msimu wa 2014/2015.
Karibu Tanzania, karibu msimbazi, karibu Afrika kocha wa mpira.