
Klabu ya soka ya Simba kutoka nchini Tanzania imeongoza kwa kufuatiliwa katika mtandao wa Instagram kwa mwezi septemba mwaka huu. Ukurasa wa Simba umetembelewa zaidi ya watumiaji millioni kumi(10 ) kwa mwezi wa tisa na kuwaacha mbali wababe wengne wa Afrika kama Al Ahly ya Misri, Mamelodi ya Afrika Kusini pamoja na watani wao wa jadi Klabu ya Yanga .
Kwa mabara mengine. Klabu ya Manchester United imeongoza katika bara la ulaya. Huku Klabu a Palmeiras ikiongoza bara la Amerika, Persib fc imeongoza bara la Asia na Melbourne city imeongoza bara la Oceania( Australia).Takwimu hizi zimetolewa na jarida maarufu duniani la deporfinanzas.