Baada ya mechi ya hatua ya pili kufuzu makundi ya Klabu bingwa barani Afrika kuchezwa mwishoni mwa wiki iliyopita. Idadi ya Timu 16 zimepatikana. Mabingwa watetezi Al Ahly ya Misri pamoja na Zamalek, Wyadad Casablanca , Raja Casablanca, Mamelodi Sundown, El Merrekh, Al Hilal, ni baadhi ya vugogo waliotinga hatua ya makundi.
Klabu za Tp Mazembe, As vita club Klabu za Congo Drc zimeshindwa kufuzu hatua ya makundi za michuano ya Klabu bingwa Afrika, pamoja na Klabu ya Simba ya Tanzania .