Nyota wa klabu ya Asec Mimosas ya nchini Ivory coast Stephane Aziz Ki amegeuka lulu kuelekea dirisha kubwa la usajili baada ya kutakiwa na vilabu vikubwa barani Afrika.
Nyota huyo aliyekuwa akihusishwa na klabu za Simba na Yanga ameripotiwa kuwa kwenye mazungumzo na Klabu yake ya kuongeza mkataba wa mwaka mmoja huku taarifa kutoka nchini Ivory Coast zikiripoti Asec Mimosas kukataa ofa kutoka Klabu ya Tp Mazembe.
Hata hivyo Wakala wa mchezaji huyo ameweka wazi kuwa sio Tp Mazembe tu wanaomtaka Azizi Ki bali Mamelodi Sundowns na Kaizer Chiefs zote za Afrika Kusini zimeonesha nia ya kutaka huduma yake.
Mpaka sasa Pyramids ya nchini Misri ndiyo inayopewa nafasi kubwa ya kumsajili nyota huyo na wamemtengea ofa nono na mkataba wa miaka mitatu.
Wakala wake amesema kilichopelekea ofa ya Mazembe kupigwa chini ni kushindwa kuweka ofa mezani waliyowaambia.
Awali Yanga iliripotiwa kufikia pazuri hata hivyo imeonekana itakumbana na nguvu kubwa ya pesa kutoka kwa matajiri hao wa Misri
