Mshambuliaji wa Barcelona na Timu ya Taifa ya Gabon, Pierre Emerick Aubameyang ametangaza kustaafu soka la Kimataifa na Gabon akiwa na umri wa miaka 32.
Aubameyang ambaye amekuwa nahodha wa timu ya Taifa ya Gabon amehudumu katika kikosi hicho kwa kipindi cha miaka 10 akicheza mechi 72 huku akifunga magoli 30.
