Leo hii Klabu ya Simba imemtangaza Ahmed Ally kuwa afisa habari na mawasiliano. Nafasi hii ilikua wazi tokea aliyekua afisa habari wa Simba kwa miaka zaidi ya mitano Haji Sunday Manara kusitishiwa mkataba wake.
Ahmed Ally ni mtangazaji nguli wa Azam TV ni matumaini ya wanasimba na wapenda mpira kwa ujumla kwamba ataitendea haki nafasi aliyopewa.
Baada ya Manara kuondoka nafasi hii alikaimu Ezekiel Kamwaga kwa ufanisi mkubwa kwa kipindi cha miezi miwili na baada ya hapo Ally chantry( chico) alikaimu nafasi hiyo Hadi mwishoni mwa mwaka Jana. Hadi sasa Klabu ya Simba ipo nafasi ya pili kwenye Ligi kuu, na mwezi wa pili itaanza kucheza hatua ya makundi kombe la Shirikisho barani Afrika.

