
BAROBARO ADAIWA MBELE YA WAKWE ZAKE
Mzee mmoja kutoka eneo la Chepalungu alikosa amani na
kuchemka kwa hasira baada ya wanaume wawili
wanaomdai walipoamua kumvamia siku yake ya kulipwa
mahari na kutaka awalipe
Penyenye zinaarifu kwamba jamaa alikuwa na raha isiyo na
kifani siku hiyo kwani alitarajia donge nono kama mahari
baada ya bintiye kuolewa.
Kulingana na Taifa Leo, wageni wa lofa walifika na
akawapa mapokezi ya kishua nao wakajawa na furaha mno
kwa makaribisho Inaarifiwa kwamba jamaa alipotishiwa
kuwa atachukuliwa hatua za kisheria hivi majuzi aliahidi
kuwa angelipa deni hilo akikabidhiwa mahari ya binti yake.
Hata hivyo, alipandwa na hasira wageni wake walipofika na
kumdai akiwa na wageni.
