Winga wa Klabu ya Namungo Fc Shiza Ramadhan Kichuya amelalamika kutukanwa na baadhi ya mashabiki wa Klabu ya Yanga wakimtuhumu kuwa ana jezi ya mshambuliaji wa Klabu ya Yanga Fiston Mayele ambayo wazee wamekuwa wakiitaka
Shiza Kichuya amekanusha kuwa yeye hakubadilishana jezi na Fiston Mayele bali alibadilishana jezi na Denis Nkane.
Siku za hivi karibuni zimeibuka taarifa kuwa kuna mchezaji alibadilishana jezi na Mayele akaondoka nayo ikiwa bado na jasho na kwenda kuitumia kumroga mshambuliaji huyo ambaye ana mabao 12 mpaka sasa.
Taarifa tulizozipata ni kwamba aliyebadilishana jezi na Mayele ni mtoto wa Kocha wa Namungo Super Kihwelo
