Klabu ya Simba imepanga kupitisha panga kwa nyota wake kadhaa ili kuongeza wachezaji wapya kwajili ya kuimarisha kikosi chao kwajili ya msimu ujao wa ligi kuu ya NBC na michuano ya kimataifa.
Awali Simba haikupanga kuacha wachezaji wengi, lakini baada ya kushindwa kufikia malengo yao msimu huu wameamua kukisuka upya kikosi chao ili kiweze kufanya vizuri zaidi kwenye michuano ya Kimataifa ikiwemo kuvuka hatua ya robo fainali jambo ambalo limekuwa mtihani mkubwa kwao kwenye miaka hii ya karibuni.
Mmoja wa vigogo wa Simba ambaye hakutaka jina lake litajwe amesema Simba wameamua kukiimarisha Kikosi chao kwa kufanya usajili wa maana bila mihemko ili kufikia malengo yao.
Nyota wanaotajwa kupewa mkono wa kwaheri ndani ya Klabu ya Simba ni :-
Chris Mugalu
Meddie Kagere
Pascal Wawa
Taddeo Lwanga na
Bernard Morisson
Wachezaji wenye asilimia 50/50 za kubaki ama kuondoka ni pamoja na
Peter Banda
Pape Ousmane Sakho
Rally Bwalya
Ally Salim
Gadiel Michael
Jimmyson Mwanuke
Erasto Nyoni
Yusuph Mhilu.
