Beki wa kulia wa Klabu ya soka ya Yanga ya nchini Tanzania Kibwana Shomari ameongeza Mkataba wa miaka miwili kuendelea kusalia katika klabu hiyo yenye maskani yake mitaa ya Twiga na Jangwani.
Beki huyo ambaye ana uwezo wa kucheza kama beki wa kushoto pia amekuwa akiwindwa na timu kadhaa zikihitaji huduma yake baada ya mkataba wake kuelekea ukingoni
Hata hivyo leo ameongeza mkataba mpya na ataendelea kusalia jangwani.
