
Polisi ajipiga risasi kwa bahati mbaya akimenyana na mhalifu
Kachero wa Kituo cha Polisi cha Parklands katika Kaunti ya Nairobi alijipiga risasi na kujijeruhi.
Kachero huyo kwa jina Luke Juma anauguza jeraha la risasi katika hospitali moja jijini Nairobi baada ya kujipiga risasi kwa bahati mbaya alipokuwa akimtia mbaroni mshukiwa mnamo Ijumaa Oktoba 29.
Kulingana na ripoti iliyoonekana na TUKO.co.ke, Juma alikuwa akimkimbiza unyounyo mshukiwa hatari wa uhalifu anayetambulika kama Philiph Munyasia. Inadaiwa Munyasia aligeuka na kuwa mtoro baada ya kutekeleza kisa kilichomwacha mtu akipigania uhai wake.
Mshukiwa alikimbia kwa kasi nyuma ya Juma huku akiruka mashimo yaliyojaa matope na mitaro huku akifuatwa kwa karibu na kachero huyo. Alijeruhiwa kwenye mguu wake wa kushoto, juu ya goti lake baada ya risasi hiyo kupenyeza hapo.
