
PICHA|Hisani
Christiano Ronaldo amepokea Tuzo lake la kwanza baada ya kujiunga Tena na Klabu ya Manchester United hii Ni baada ya kutawazwa kuwa Mchezaji Bora wa Klabu hiyo Mwezi wa Septemba.Ronaldo alijiunga Tena na Klabu ya Manchester United Mwezi wa Agosti akitokea Klabu ya Juventus.
Mshambulizi huyo wa Ureno ameifungia Manchester United Mabao Tano Katika mechi Tano ambazo amecheza Tangu kurejea kwake.Mabao matatu ameyafunga Katika Ligi kuu ya Uingereza na Mabao mawili akayafunga Katika Michuano ya Klabu Bingwa Barani Ulaya.
Ronaldo pia ameteuliwa miongoni mwa wale wachezaji ambao huenda wakatangazwa Kama wachezaji Bora Mwezi Septemba kwenye Ligi kuu ya Uingereza.Baadhi ya wachezaji walioteuliwa pia Ni Mohammed Salah wa Liverpool,Antonio Rudiger wa Chelsea,Ismaila Sarr wa Watford,Allan Saint-Maximin wa Newcastle Kisha na Jao Cancello wa Klabu ya Manchester City.
