Shirikisho la soka Barani Afrika limeipiga faini Klabu ya Simba Usd 10,000 (Tsh Milioni 23) kwa kitendo cha kuwasha Moto kwenye mchezo wa pili wa robo fainali uliopigwa nchini Afrika Kusini dhidi ya Orlando Pirates
Shirikisho la soka nchini Afrika Kusini SAFA waliwatuhumu Simba wakiwahusisha na imani za kishrikina na kuandika malalamiko yao Shirikisho la soka Barani Afrika.
Katika mchezo huo, Simba walipoteza kwa bao 1-0 bao lililofungwa na Kwame Peprah na kupelekea mchezo kwenda hatua ya mikwaju ya penati na Simba kutolewa.
