
Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi ya Tanzania, George Simbachamwenge amesema kuwa serikali imempatia uraia wa Tanzania mashambulizi wa klabu ya Simba Sc,Kibu Denis kwa mujibu wa Sheria ya Uraia,Sura 357 (Rejeo la 2002),baada ya kupokea ombi kutoka TFF kupitia Wizara ya Sanaa,Utamaduni na Michezo.
Waziri Simbachamwenge amesema uraia wa asili wa Kibu Denis alikuwa raia wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo (DRC), lakini amekuwepo nchini Tanzania tangu mwaka wa 1998,akiwa na umri wa miaka sita,baada ya wazazi wake kukuambia machafuko ya kisiasa nchini humo.
Ameongeza kuwa mchezaji huyo amekuwa na nyaraka zinazoonyesha ni raia wa Tanzania, iliwemo kitambulisho cha uraia,kwani yeye alikuwa anajijua ni Mtanzania kutokana na kuongia nchini akiwa na umri mdogo,na hana historia yoyote na nchini yake ya asili zaidi ya kukalia Tanzania.
