Rita Dominic aolewa kwa mara ya Kwanza akiwa na miaka 46. Mwigizaji huyo maarufu wa Nigeria amefunga ndoa ya kiasili na muonekano wake ni huo.

Ameolewa na Fidelis(56) ambaye amewekeza maeneo kadhaa ikiwemo katika tasnia ya habari. Wamekuwa pamoja kwa miaka kadhaa kabla ya kuoana Sasa
Rita aliwahi kusema angependa kuolewa na anaheshimu ndoa ila hana haraka hadi muda wake ufike anataka aingie kwenye ndoa moja kwa moja sio kuharakisha na kuishia kuolewaolewa
Amesema ndoa ni muhimu ila Kuna wakati inakera kwa jinsi watu walivyoweka mkazo kwenye ndoa na hivyo kusababisha watu kupata presha kubwa na kuingia kwenye ndoa kufurahisha watu na zinaishia kuvunjika
Rita Dominic licha ya umri alionao bado hajazaa mtoto wake mwenyewe isipokuwa aliwahi kusema analea watoto ambao si wake na analea watu wengine kwahiyo haoni tatizo ila angependa Mungu ambariki mtoto wake siku moja
Inadaiwa Rita ana tatizo la Endometriosis ambalo hupelekea kupata ugumba kirahisi kwa wanawake mbalimbali lakini hajawahi kuligusia hilo kwa ndani ingawa amekuwa akielemisha jamii kuhusu tatizo la Endometriosis na hata mwanamitindo wa kimataifa toka Tanzania, Millen Magese aliwahi kusema alipata hamasa toka kwa Rita Dominic kujitokeza ili kuzungumzia tatizo hilo jamii ipate elimu
Kwenye comments section kuona picha zaidi, ikiwemo mume wake.
