
Karua anampiku Waiguru kama mgombea anayependelewa kuwa naibu rais katika Mlima Kenya.
Kiongozi wa chama cha NARC Kenya Martha Karua ameibuka kuwa chaguo bora kuwa Naibu Rais katika mkoa wa Mlima Kenya kulingana na utafiti uliofanywa na kutolewa hivi karibuni na Mizani Afrika.
Katika taarifa iliyowekwa hadharani Jumatatu, Oktoba 18, Karua alichaguliwa kama mgombea wa kike anayeweza kuwa manaibu wa rais na kiwango cha umaarufu cha hasiliamia 34.8% Karua anafuatwa kwa karibu na Agnes Kagure na Gavana wa Kirinyaga Anne Waiguru na kiwango cha umaarufu cha asilimia 31.9 na 14.9 mtawaliwa.
Mnamo Septemba,Shirika la Mizani Afrika pia ilimtaja Karua kama mwanasiasa mwenye ushawishi mkubwa kutoka eneo la Mlima Kenya akifuatiwa na gavana Waiguru.
