
Timu ya Taifa ya Mali almaarufu Kama The Eagles ilikatiza Ndoto ya Timu ya Kenya Harambee Stars ya kushiriki kwenye Dimba la Kombe la Dunia Mwaka 2022 kule Qatar.Ndoto hiyo ilizimwa hapo Jana Jumapili,10 Oktoba baada ya Mali kuwacharaza Vijana wa Harambee Stars uwanjani Nyayo jijini Nairobi.
Mechi hiyo ilikuwa ya mkondo wa Pili siku chache baada ya Mkondo wa kwanza kuchezwa kule Morocco ambapo Timu ya Mali iliweza Tena kuibuka mshindi wa hatua hiyo ya kwanza baada ya kuilaza Harambee Stars Mabao Tano kwa Bila.
Kwenye mkondo wa Pili jijini Nairobi,Kenya walijaribu kuonyesha mchezo mzuri wakiongozwa na kocha wao Engin Firat lakini mwishowe waliishia kupoteza mechi hiyo.Mshambulizi wa Timu ya Mali Ibrahima Kone ndiyo alifunga bao la pekee mchezoni dakika ya 55.Ibrahima pia aliweza kucheka na wavu Mara tatu kule Agadir,Morocco kwenye mechi ya mkondo wa kwanza.
Kwa Sasa Mali ndio wanaongoza kundi E kwa alama Kumi huku Uganda wakifuatia na alama name baada ya kupata ushindi wa Bao moja kwa Nunge dhidi ya Vijana wa Rwanda.Kenya ipo Katika nafasi ya tatu na alama mbili huku Rwanda wakifunga kundi na alama mbili pekee.
