Mwalimu wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars Kim Poulsen amefanya marekebisho madogo katika kikosi cha leo . Beki Kennedy Juma ameanza pamoja na mshambuliaji Kibu Dennis wakichukua nafasi ya John Bocco ambaye ameanzia benchi pamoja na Mzamiru Yassin ambaye anatumikia kadi ya njano. Tanzania inasaka kulipa kisasi baada ya juzi alhamisi kufungea na Benin katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam
