
Babrisky ataja sababu za kujibadilisha
kuwa mwanamke
Idris Okuneye, ambaye anafahamika kwa wengi kama
Bobrisky ni mmoja wa watu maarufu sana nchini Nigeria ,
Bobrisky alizaliwa mwanamume na sasa anataka
kujibadilisha kuwa mwanamke.Instagram Mnigeria huyo
alisisitiza kuwa anataka kujisimamia mwenyewe akitumia
alichonacho kupata anachotaka bila kujali wanaomsema
Kulingana na celeb huyo, kabla ya kubadilisha jinsia,
alikuwa maskini na hakuna aliyeshughulika naye kando na
mama yake pekee. Lakini alichoshwa na hali hiyo na
kutaka kuwa mtu anayejisimamia mwenyewe
Mnamo Julai 8, 2021, Bobrisky alianika mwili wake
mitandaoni kuonyesha muonekano wake mpya baada ya
kufanyiwa upasuaji wa kubadilika kuwa mwanamke.
Bobrisky alianza kugonga vichwa vya habari mnamo Mei
2019, alipojitokeza hadharani akitaka atambulike kama
mwanamke na wala si mwanamume. Hata hivyo, uamuzi wake ulipokelewa na hisia mseto mitandoani huku baadhi
wakimdhihaki na wengine wakidai ana uhuru na uamuzi
wake unatakiwa kulindwa
Kulinga na ripoti ya Google mwaka 2016, Bobrisky ndiye
anaongoza kama mtu aliyesomwa na kutafutwa sana
kupitia Google nchini Nigeria.
